Back to top

Yanga yasema Benard Morrison ni mchezaji halali wa timu hiyo.

01 October 2020
Share

Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia kwa makamu mwenyekiti wake Fredrick Mwakalebela umesema kuwa Mkataba wa mchezaji Benard Morrison na klabu ya Simba unamapungufu hivyo Benard Morrison ni mchezaji halali wa Yanga.

Akizungumza na waandishi wa habari Fredrick Mwakalebela amesema Simba wameweka mkataba huo katika mfumo wa usajili wa FIFA TMS na hivyo unamapungufu ambayo ni pamoja na kutokuwa na saini ya kiongozi yoyote wa klabu hiyo zadi ya saini ya Benard Morrison.

Hivyo mkataba huo haujakubalika na FIFA kwa mujibu wa Fredrick Mwakalebela, Benard Morrison bado ni mchezaji wa Yanga.

Swali ni Je Simba watakatwa pointi katika mechi zote alizocheza Morrison?.