Back to top

Zitto Kabwe na wenzake 4 wanaletwa Dar kwa matibabu.

07 October 2020
Share

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Ndg.Zitto Zuberi Kabwe pamoja na majeruhi wengine 4 waliopata ajali ya gari jana Oktoba 6, 2020 katika Jimbo la Kigoma Kusini wanatarajia kuwasili Dar es Salaam majira ya saa 5:00 asubuhi katika Uwanja wa Ndege wa zamani Terminal 1.

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Ndg.Zitto Zuberi Kabwe

Baadaye majeruhi wote watapokelewa na gari la wagonjwa na kupelekwa hospitali kwa matibabu zaidi.

Mbali na Zitto, majeruhi wengine ni pamoja na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, Said Rashid Bakema, Katibu wa Jimbo la Kigoma Kusini, Soily Simon Matete pamoja na Boaz Chuma, (mwanachama).

Muonekano gari aliyopata nayo ajali Kiongozi wa ACT Wazalendo Ndg.Zitto Kabwe na wenzie 4  wakati akiwa katika Jimbo la Kigoma Kusini kwa ajili ya mkutano wa kampeni jana Oktoba 6, 2020.

Taarifa zaidi zitakujia.