Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), limesema kumetokea hitilafu kwenye mfumo wa njia ya kusafirisha umeme ya Gridi ya Taifa, hali ambayo imesababisha baadhi ya maeneo nchini kukosa huduma ya umeme.
.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Shirika hilo imeeleza kuwa hitilafu hiyo imetokea majira ya Saa 8:22 Usiku, na kwamba wataalamu wake wanaendelea na jitihada za kurejesha huduma hiyo.