Back to top

TANESCO: MITAMBO YA KIDATU ILIJIZIMA ILI KUJILINDA

01 April 2024
Share

Shirika la Umeme nchini (TANESCO), limesema sababu iliyosababisha kutokea kwa athari kwenye mfumo wa Gridi ya Taifa ni hitilafu kwenye mfumo wa kudhibiti kiwango cha maji kwenye mitambo ya kufua umeme ya Kidatu na hivyo kushindwa kuzuia mtiririko mkubwa wa maji yanayoingia kwenye mitambo na kusababisha mitambo hiyo kujizima kwa ghafla ili kujilinda jambo lililosababisha athari kwenye mfumo mzima wa Gridi ya Taifa.
.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Shirika hilo imesema, tayari mitambo ya kudhibiti uingizaji maji kwenye Kituo cha Kidatu, iliyopata hitilafu imebadilishwa na kuwekwa mingine na kazi ya kutoa maji yaliyoingia kwenye vyumba vya kuendesha mitambo inaendelea pamoja na kuanza taratibu za kuwasha mitambo ya kufua umeme. 
.
Kufuatia adha hiyo TANESCO imewaomba radhi wateja wake wote na umma kwa ujumla.