Back to top

GEN Z UGANDA WAJITOKEZA KUANDAMANA

23 July 2024
Share

Baadhi ya vijana nchini Uganda, wamejitokeza mtaani kutekeleza adhma yao ya kuandamana kwa ajili ya kupinga vitendo vya rushwa na ufisadi serikalini.

Polisi waliovalia mavazi ya kiaskari wa kutuliza ghasia na wengine sare za kivita, wamesambaa katika mitaa ya Jiji la Kampala pamoja na kuweka vizuizi barabarani, lengo kuhakikisha hali ya usalama inaimarika lakini kuhakikisha vijana hao hawaandamani.

Msemaji wa Polisi nchini humo, Kituuma Rusoke, amesema mamlaka nchini humo hazitaruhusu maandamano yatakayohatarisha amani na usalama wa nchi.

Siku chache zilizopita Rais wa nchi hiyo, Yoweri Museveni aliwaonya wananchi wanaopanga maandamano, yanayolenga kupinga vitendo vya #Rushwa nchini humo, wengi wao wakiwa ni Vijana wa 'Gen Z'

Museveni alisema "Una haki gani unayotafuta kwa kuleta machafuko?, tuna shughuli nyingi za kuzalisha mali, unapata chakula cha bei nafuu, sehemu nyingine za dunia wanakufa njaa wewe hapa unataka kutuvuruga? unacheza na moto, hatuwezi kukuruhusu utusumbue"