Back to top

MOTO WATEKETEZA VIBANDA MSAMVU MOROGORO

24 July 2024
Share

Moto umeteketeza vibanda zaidi ya kumi vya wafanyabiashara, vilivyopo pembeni mwa Kituo Kikuu cha Mabasi cha Msamvu mjini Morogoro na kusababisha hasara ikiwemo ya uharibifu wa mali.

Baadhi ya Wafanyabiashara na mashuhuda wa tukio hilo, wamesema hadi sasa chanzo cha moto huo hakijajulikana  ingawa miongoni mwa vibada hivyo kibanda kimoja kilikutwa na jiko la mkaa likiwa linawaka.

Kwaupande wake Afisa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro, Mrakibu Msaidizi (ASF), Daniel Myalla, amesema waaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha moto huo na wamefanikiwa kuudhibiti usiendelee kuleta madhara kwenye vibanda vilivyo katika maeneo hayo.