Back to top

POLISI WAJENGEWA UWEZO UKAGUZI WA MITAMBO MIZITO

25 July 2024
Share

Chuo cha Mitambo mizito (IHET) kimetoa mafunzo kwa askari wa Jeshi la Polisi, ambapo awamu hii kimeweza kutoa mafunzo ya ukaguzi wa mitambo mizito, huku washiriki wakibanisha kuwa utaalam huo walioupata unakwenda kuongeza ufanisi katika ukaguzi wa mitambo hiyo.

Akiongea mara baada ya mafunzo hayo Mkuu wa Chuo cha Mitambo Mizito (IHET), Asia Ntembo amesema kuwa lengo la chuo hicho ni kuwajengea uwezo askari wa Jeshi la Polisi katika ukaguzi wa mitambo mizito huku akibanisha kuwa chuo hicho kimebobea katika kutoa mafunzo hayo.

Asia meongeza kuwa taasisi na makampuni mbalimbali wahakikishe watendaji wao wamepata mafunzo ya kutumia mitambo mizito ambapo amewataka wahusika kushiriki katika mafunzo ili wawe na uelewa katika matumizi ya mitambo hiyo.

Kwa upande wake mkufunzi kutoka chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) Mrakibu wa Polisi SP Seni Magembe amesema kuwa mafunzo waliyoyapata yamewajengea uwezo huku akibainisha kuwa mafunzo hayo yanakwenda kuwa suluhuisho ya maarifa yaliyokosekana katika ukaguzi wa mitambo mizito.

Naye Mkufunzi kutoka chuo cha mitambo mizito IHET Robert Mrema amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo wakaguzi wa magari wa Jeshi la Polisi ili kuwa na ufanisi katika ukaguzi wa mitambo mizito.

Mhitimu wa mafunzo ya mitambo mizito Mkaguzi msaidizi wa Polisi A/INSP Elibariki Tile amebainisha kuwa mafunzo hayo yamewajengea katika utambuzi wa mitambo hiyo huku akiweka wazi kuwa wamejifunza namna ya kufanya kazi kwa mitambo hiyo.