
Siku mbili baada ya kuzindua kampeni ya msaada wa kisheria wa Mama Samia Mkoani Lindi wananchi wa halmashauri ya Manispaa ya Lindi wametoa shukrani zao kwa Rais wa Jahuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwapelekea huduma hiyo ambayo imekuwa msaada katika ufumbuzi wa matatizo yao ya kisheria.
Wakizungumza wakati wa kupata huduma hiyo wananchi wa mitaa ya Mtele, Mmakonde na Sokoni Kata ya Mingoyo wamesema kampeni hiyo imekuwa msaada kwao Katika kupata ufumbuzi wa matatizo yao.
Mratibu wa kampeni hiyo katika Manispaa ya Lindi, Hosana Mgeni, amesema kampeni hiyo ya msaada wa kisheria kwa Manispaa hiyo itafikiwa ikihusisha mitaa 10 kwa kila Kata hizo.
Katika kampeni hiyo licha ya kutatua na kusikiliza matatizo ya wananchi pia maafisa hao wametoa elimu mbalimbali juu ya maswala ya aridhi, ndoa, mirathi na ukatili wa kijinsia na umuhimu wa kuacha wosia.