
Jeshi la Polisi katika mkoa wa Kagera kupitia kitengo chake cha usalama barabarani kwa kushirikiana na wadau mbalimbali mkoani humo limeanza kuwahamaisha madereva waliojipatia leseni za udereva bila kupata mafunzo ili wachukue hatua za haraka za kujiunga na vyuo vinavyotoa mafunzo ya udereva jambo litakalowajengea uwezo wa kuelewa kanuni na sheria ambazo wanapaswa kuzifuata wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto.
Jeshi hilo kwa kushirikiana na wadau limefanya uhamasishaji huo kwenye ukumbi wa Linas uliko katika manispaa ya Bukoba kwa kukutana kwa baadhi ya waendesha vyombo vya moto ambavyo ni pamoja na magari na pikipiki waliojipatia leseni za udereva bila kuhudhuria mafunzo yoyote, akizungumza wakati wa uhamasishaji huo mwenyekiti wa zamani wa kamati ya usalama barabarani ya mkoa wa Kagera Winston Kabantega amesema lengo la kuwahamasisha waendesha vyombo vya moto waliojipatia leseni za udereva bila kuhudhuria mafunzo ni pamoja na kupunguza ongezeko la ajali na afisa wa kikosi cha usalama barabarani Bw.Andrew John akizungumza amesema kikosi hicho kimejipanga vizuri katika kuwadhibiti madereva wasio na sifa za kuendesha vyombo vya moto.
Kwa upande wao baadhi ya waendesha vyombo vya moto walioudhuria uhamasishaji huo wamepongeza juhudi zinazofanywa jeshi la polisi mkoani Kagera linaloshirikian na wadau katika kuweka mikakati ya kukabiliana na ajali hasa zile ambazo uchangiwa na uzembe wa madereva, kwa nyakati tofauti wamesema mafunzo ya udereva yatawajengea uwezo wa kujiepusha na ajali ambazo huchangiwa na uelewa mdogo walionao madereva juu ya kanuni na sheria za usalama barabarani.