Back to top

Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kutumia ipasavyo vivutio vya utalii.

24 August 2018
Share

Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini imejipanga kutumia ipasavyo vivutio vya utalii vilivyopo na fursa ya Maonesho ya Utalii Karibu Kusini kuwa nguzo ya uchumi wa viwanda na ajira kwa wananchi wa mikoa hiyo.

Ofisa Utalii Mkoa wa Iringa, HAWA MWECHAGA amebainisha hayo kwenye kikoa cha wadau wa Utalii Karibu Kusini na kusema mikoa hiyo ina vuvitio vya kipeke vya utalii ambavyo vikiimarishwa vinaweza kukuza uchumi na ajira kwa wananchi wake.

Akizungumza kwenye kikao hicho, Mkuu wa Kanda, Ofisi ya Utalii Kusini, Ofisa Utalii huyo amewataka wananchi wa mikoa hiyo kuchangamkia fursa za utalii kwa sababu serikali imeanza kutatua matatizo ya miundombinu duni iliyo kuwa inakwamisha maendeleo ya utalii katika ukanda huo.

Mwenyekiti wa kikao hicho, Bwana RICHARD KASESELA amehimiza umuhimu wa ushirikiano kwa wadau wote wa utalii katika mikoa hiyo ili kuharakisha maendeleo ya utalii katika mikoa hiyo.