Back to top

Dawa mseto bado haijashindwa kutibu vimelea sugu vya malaria nchini.

12 November 2018
Share

Jopo la wanasayansi na watafiti wa masuala ya afya ya jamii kutoka Chuo Kikuu Katoliki cha Sayansi za afya Bugando ( CUHAS ), wamewahakikishia wananchi hususani waishio mikoa ya kanda ya Ziwa kwamba dawa mseto ya malaria yenye mchanganyiko wa dawa mbili, haina madhara kiafya na pia inatibu vimelea sugu vya ugonjwa huo kwa zaidi ya asilimia 90.

Mkurugenzi wa Elimu za juu Chuo kikuu katoliki cha sayansi za afya Bugando Prof. Erasimus Kamugisha, akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza, amesema tafiti zao zinaonyesha kuwa dawa mseto ya aluu inafanya kazi vizuri, ni salama na inatibu malaria kwa kiwango cha kutosha na pia haina usugu wa vimelea vya malaria tofauti na inavyodaiwa na baadhi ya watu katika jamii.