
Waziri wa kilimo Mhe Josephat Hasunga amesema serikali bado inaendelea na zoezi la uhakiki wa wakulima wa zao la korosho na kuwaondoa waliofanya udanganyifu ili kuendelea kuwalipa fedha zao kihalali ambapo mpaka sasa imefanya uhakiki wa vyama vya msingi wakulima 466 huku ikiwahakikishia wakulima wote kulipwa fedha zao mara baada ya kukamili kwa zoezi la uhakiki.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Waziri Hasunga amesema serikali mpaka sasa imekusanya zaidi ya tani laki moja kutoka kwa wakulima wa zao la korosho ambapo amesema wapo baadhi ya wakulima ambao wameshindwa kupata fedha kutokana na taarifa zao za kibenki kuwa na mkanganyiko.