Wananchi wa manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wamelalamikia ubovu wa stendi kuu ya mabasi ya Msamala wilayani Songea ambapo wameiomba serikali kutengeneza stendi hiyo na kuwaondolea adha wananchi.
Wananchi wakiwemo madereva na makondakta ambao magari yao yanapitia katika kituo kikuu hicho cha mabasi yaendayo mikoani wanasema kutokana na mashimo katika stendi hiyo na ubovu wa barabara za kuingilia stendi magari yao yamekuwa yakiharibika
Kwa aupande wao abiria wanasema kuwa uchafu katika stendi hiyo ni changamoto nyingine na pia vyoo havitoshelezi.
Akijibu malalamiko hayo mkurugenzi mtendaji wa manispaa ya Songea Bi.Tina Sekambo amekiri kituo hicho cha mabasi Songea kukabiliwa na changamoto lukuki na kwamba wametenga milioni 70 za ukarabati.