
Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi,Bw.Christopher Ngubiagai, amewataka wananchi wilayani humo,ambao bado wako mashambani maeneo ya mabondeni kuondoka mara moja katika maeneo hayo kwani mvua zinanyesha bado na zitaendelea kunyesha kwenye maeneo mbalimbali wilayani Kilwa.