Back to top

Soka haliwezi kupiga hatua kwa kutegemea 'chungu cha maji'-Mwakyembe

14 February 2020
Share

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania, Dkt.Harrison Mwakyembe amesema kwamba mchezo wa mpira wa miguu nchini Tanzania hauwezi kusonga mbele kama fikra potofu hazitaondolewa na kuendelea kutawala kwenye mchezo huo, kwa imani kwamba ushindi lazima upatikane kwa 'kalumanzira'. 

"Tunapata tabu sijui tutumie njia gani kuondoa fikra hizi kichwani za kwamba ushindi hauji tu ndani ya soka lakini kuna jamaa anaweza akachezesha kwenye sijui chungu cha maji ukashinda mechi haiwezekani"-Waziri Mwakyembe


Akizungumza katika kipindi cha Meza Huru kinachorushwa na ITV Waziri Mwakyembe amegusia mambo mengi katika mustakabali wa soka la Tanzania na hatua za kusonga mbele kimataifa, hukua akisema kuwa Uingereza ishajiandaa kwamba soka kwao ni biashara lakini kwa Tanzania bado.

"Utajengaje msingi Imara wa wachezaji wa ndani,ukiendelea kutegemea wachezaji wa nje?,Tunaiga Uingereza wenzetu walishafanya maamuzi kwamba soka kwao ni biashara kila kitu kimeelekea kule, lakini sisi hatujajianda chochote".Waziri Mwakyembe.

Amesema ushindi wowote ule katika soka unatokana na kufanya mazoezi na si vinginevyo kwani hakuna muujiza wowote unaoweza kuleta matokeo bila kujituma.

"Bila kuwa na mazoezi ya kutosha huwezi kufanikiwa kwenye soka, tunapata tabu sana kama kuna mechi ya hizi timu kubwa, tunatumia askari zaidi ya 50 kwa siku kuzuia watu usiku wanakesha, wanapanda ukuta mara sijui watupe yai"Waziri Mwakyembe

Waziri Mwakyembe ameongeza kuwa timu zinazoshiriki katika ligi kuu zinabajeti hivyo anataka kuondoa zile bajeti zisizo rasmi za chini ya meza.

"Timu zetu zinazohusika katika Ligi kuu na madaraja mbalimbali wana bajeti kabisa za waamuzi,sio za juu ya meza za chini ya meza,sasa tunataka ya chini ya meza itoke iwe ya juu ya meza tuweze kuwalipa wenzetu vizuri nao wajisikie wako kwenye eneo muhimu".Waziri Mwakyembe.
Tunapata tabu,wanapanda ukuta watupe yai".Mwakyembe