Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Ndg.Zitto Zuberi Kabwe pamoja na majeruhi wengine 4 waliopata ajali ya gari jana Oktoba 6, 2020 katika Jimbo la Kigoma Kusini wanatarajia kuwasili Dar es Salaam majira ya saa 5:00 asubuhi katika Uwanja wa Ndege wa zamani Terminal 1.
Baadaye majeruhi wote watapokelewa na gari la wagonjwa na kupelekwa hospitali kwa matibabu zaidi.
Mbali na Zitto, majeruhi wengine ni pamoja na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, Said Rashid Bakema, Katibu wa Jimbo la Kigoma Kusini, Soily Simon Matete pamoja na Boaz Chuma, (mwanachama).
Taarifa zaidi zitakujia.