Wakati kikosi cha Simba kikitarajia kuwavaa AS Vita kesho kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa mkoani Dar es salaam katika mchezo wa tano kundi A ligi ya Mabingwa Afrika wanachama na wapenzi wa klabu ya Simba walioko Zanzibar wamekutana leo na kufanya dua ya pamoja kuiombea timu yao iibuke na ushindi ili kutinga hatua ya robo fainali katika michuano hiyo.
Simba wanaongoza kundi hilo wakiwa na alama 10 huku wakisaka alama 1 tu kutinga hatua ya robo fainali.
MSIMAMO WA KUNDI A
1. Simba Point 10
2. Al Ahly Point 7
3. AS Vita Point 4
4. Al Merrikh Point 1