
Kamati iliyoundwa kuchunguza sakata la makontena mawili yaliyokutwa na mchanganyiko wa Korosho na Kokoto nchini Vietnam imewasilisha ripoti yake ikithibitisha hilo kufanyika na kuwepo kwa kontena bandarini lenye mchanga badala ya Korosho nalo likiwa safarini kupelekwa nchini Vietnam.
Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo yenye wajumbe tisa Bw.Khasim Mbofu amesema kamati hiyo ilipata uhakika kuwa makontena hayo yakitoka newala mkoani Mtwara ambapo madhaifu yaliyopo katika usafirishaji wa Korosho kutoka katika maghala mpaka mlaji yanachangia hayo.
Bw.Mbofu amesema katika ripoti hiyo wamebaini pia kuwepo kwa mapungufu katika bandari ya Dar es Salaam kwenye mashine za kuchunguza vilivyopo katika makontena ambapo ni jambo la kawaida Korosho na Kokoto kuonekana vinafanana.
Naye Waziri wa kilimo Dkt.Charles Tizeba amemuagiza katika mkuu wa wizara hiyo kumtaarifu mkuu wa jeshi la polisi kuhusiana na watuhumiwa wa sakata hilo hili waweze kuhojiwa na vyombo vya dola na ikithibitika ushiriki wao katika sakata hilo wafikishwe Mahakamani.
Katibu mkuu wa wizara ya kilimo mhandisi Mathew Mtigumwe amesema serikali haiwezi kuvumilia aibu hiyo hasa katika kipindi hicho ambacho zao la korosho limekuwa likiwanufaisha wakulima kuliko miaka mingine.