Mwili wa aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hayati Maalim Seif Sharif Hamad umewasili visiwani Zanzibar na kupokelewa na Rais wa Zanzibar Mhe. Dk. Hussein Mwinyi.
Mbali na Rais Mwinyi pia walikuwepo viongozi wengine wa serikali pamoja na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Dk Bashiru Ali.
Awali kabla ya mwili huo kusafirishwa kwenda Zanzibar kwa helipokta maalum ya jeshi mwili ibada ya kumuaga kiongozi huyo ilifanyika katika msiki wa Maamuru Upanga Dar es Salaam ambapo viongozi mbalimbali akiwemo Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe.Jakaya Kikwete alihudhuria.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na serikali marehemu atazikwa kijijini kwao Pemba.