Back to top

Mkuu wa Jeshi la Polisi Msumbiji na Tanzania wakutana kwa mazungumzo.

30 June 2019
Share


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Msumbiji Bernardino Rafael amewasili mkoani Mtwara na kukutana na Mwenyeji wake IGP Simon Sirro kujadili mustakabali wa mpaka wa Tanzania na Msumbiji ambao umekuwa ukihifadhi maharamia na hivyo kupelekea vifo vya Watanzania kumi waliouawa kwa kupigwa risasi na wengine sita kujeruhiwa.

Mkuu huyo amewasili na ujumbe wa watu zaidi ya kumi na tayari wamekutana na mwenyeji wake na kuanza kikao katika ofisi za mkuu wa mkoa wa Mtwara ambacho kitanzungumzia mustakabli wa ulinzi na usalama wa mpaka kati ya Tanzania na Msumbiji.

Hata hivyo mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewaambia waandishi wa habari kuwa mara baada ya mazungumzo hayo atatoa taarifa ya maafikiano baina ya ulinzi wa mpaka huo wa Tanzania na Msumbiji.