
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la MikidadiAabdi mkazi wa Manyoni amefariki baada ya kutumbukia kwenye kisima katika kitongoji cha Majengo wilayani Manyoni mkoani Singida.
ITV ilifika katika eneo la tukio na kukuta umati wa wananchi wakiwa na simanzi, huku mwenyekiti wa kitongoji cha Majengo Bw.Silvester Msogoti akisema kuwa majirani walisikia kishindo usiku wa saa tano cha kitu kutumbukia kwenye maji.
Kwa upande wake kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Manyoni,daktari Kitundu Jackson amethibitisha kupokea mwili wa marehemu Mikidadi Abdi
Mji wa Manyoni kutokana na kuwa na shida ya maji hasa nyakati za kiangazi ,wananchi wengi wamekuwa na utaratibu wa kuchimba visima kwenye nyumba zao,jambo ambalo idara inayo shughulikia mazingira ya halmashauri ya Manyoni huwataka wananchi kuhakikisha wanachukuwa tahadhari ya usalama. ambapo tayari wao wenyewe wameshaanza kuchangia nguvu zao.