![](https://www.itv.co.tz/sites/default/files/styles/large/public/field/image/jk_0.jpg?itok=Y9YVTg06)
Waziri wa Afya Dkt.Dorothy Gwajima amewataka wamiliki wa vyuo vya Afya vinavyomilikiwa na Sekta binasi hapa nchini kuwaandaa wataalamu wa kada za afya kinidhamu ili watakapo ajiriwa wafanye kazi kwa kuzingatia maadili, uzalendo, unyenyekevu na utii wakati wa kutoa huduma kwa mgonjwa, huku akisisitiza kuwa serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na Sekta binafsi kukuza uchumi wa Taifa hivyo wamiliki wa vyuo wanawajibu mkubwa wa kusimamia nidhamu ya wanafunzi ili Taifa lipate watumishi waadilifu.