Back to top

Wananchi walalamika kucheleweshewa malipo ya fidia ya ardhi Nyagungulu

26 July 2019
Share

Wakazi wa mtaa wa Nyagungulu wilayani Ilemela mkoani Mwanza wameandamana kuelekea ofisi za halmashauri ya manispaa ya Ilemela kulalamikia ucheleweshaji wa malipo ya fidia katika kaya 369 zilizopisha upanuzi wa eneo la jeshi la wananchi kikosi cha 633, baada ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutoa kiasi cha shilingi bilioni 3 na milioni 500 kwa jeshi hilo ili zitumike kulipa fidia ya kwenye kaya hizo.

Wakizungumza na ITV nje ya eneo la ofisi za halmashauri ya manispaa ya Ilemela, wakazi hao wamedai ni zaidi ya miaka kumi sasa tangu waanze kufuatilia fidia ya kupisha maeneo yao lakini mkurugenzi wa manispaa hiyo John Wanga pamoja na watendaji wake wa idara ya ardhi na mipango miji wamekuwa wakiwapiga danadana wananchi hao.

Mwenyekiti wa kamati ya ufuatiliaji wa fidia za wananchi wa mtaa wa Nyagungulu James Masengwa, amemuomba rais Dkt. John Pombe Magufuli kuingilia kati mgogoro huo ambao umesababisha wananchi wengi wa mtaa huo kushindwa kufanya maendelezo ya aina yoyote katika ardhi hiyo kwa muda mrefu.

Hata hivyo, jitihada za wakazi hao wa Nyagungulu kumuona mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Ilemela John Wanga ili kumfikishia kilio chao hazikufanikiwa baada ya kuwa nje ya ofisi kwa majukumu mengine ya kikazi. Mbunge wa jimbo la Ilemela Dkt.Angelina Mabula akizungumzia sakata hilo amewaomba wakazi hao kuwa na subira kwani mfumo wa malipo ya serikali umebadilika kwa kupitia benki kuu