Magari matano, mawili yakiwa yamewabeba waandishi wakiwa katika msafari wa Rais Dkt.John Magufuli wakitokea Mwanza kuelekea Ukerewe kupitia wilaya ya Bunda, yamepata ajali eneo la kijiji cha Kasuguti, Wilayani Bunda mkoani Mara.
Waandishi wanne wamejeruhiwa akiwemo mmoja Tunu Herman wa gazeti la Majira, Rose Jacob Nipashe ambaye amepata michubuko, Neema Emmanuel wa Nipashe, Pius Rugonzibwa wa gazeti la Daily News.