Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa, amewataka wamiliki wa shule na madereva wa mabasi yanayotoa huduma za usafiri kwa wanafunzi wajiridhishe kuhusu njia wanazopita ili kuhakikisha kunakuwepo na usalama wa wanafunzi wanaowabeba katika vyombo vya usafiri.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ametoa Bilioni 66, kwa ajili ya kuanza urejeshaji wa miundombinu ya barabara zilizoharibika nchini.
Mabalozi wamehimizwa kutumia taaluma, uzoefu na ujuzi tofauti waliokuwa nao, kuharakisha mabadiliko ya kimfumo yanayoendelea ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Naibu Waziri Pinda amesema hayo wakati wa hotuba ya ufunguziwa Kikao cha Wadau na Tume ya Taifa ya Matumizi ya ardhi alipomwakilisha Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa kufungua Mkutano huo Jijini Dodoma.
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), imekamata jumla ya Kilogramu 767.2
za dawa za kulevya katika operesheni zilizofanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, na Tanga kuanzia
tarehe 4 hadi 18 Aprili 2024. Kati ya dawa zilizokamatwa, heroin ni kilogramu 233.2, methamphetamine
kilogramu 525.67 na skanka kilogramu 8.33........