Back to top

Wanahabari wa 4 wapata ajali katika msafara wa Magufuli Simiyu.

09 September 2018
Share

Gari la lililokuwa limebeba waandishi wa habari wa mkoa wa Simiyu limepata ajali, kwenye msafara wa Rais Magufuli Mjini Mhanuzi Wilayani Meatu, Gari hilo liligongwa na magari mengine kwa nyuma. 

Waandishi hao ni Berensi China na Masunga Samson wa ITV, Aidan Mhando (Channel Ten) na Faustin Fabian wa Mwananchi na wamekimbizwa hospitali ya wilaya Meatu kwa ajili ya matibabu, hakuna vifo.

Kwa mujibu wa kaimu mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, DktCharles Enock amesema wamepokea watu wanne na wanaendelea kuwapatia matibabu katika hospitsli hiyo.

Inaelezwa kuwa Gari lililokuwa limewabeba wanahabari liligongwa kwa nyuma na gari jingine wakati likiingia stendi ya mabasi ya Meatu.

https://www.itv.co.tz/news/wandishi-4-wajeruhiwa-katika-ajali-bunda-mkoa...