Back to top

MBAROUK SALIM ATEULIWA KUWA MAKAMU M/KITI NEC

29 June 2023
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ambapo amemteua Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Mbarouk Salim Mbarouk kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo kwa kipindi cha pili.
.
Mhe.Rais Samia pia amemteua Wajumbe wawili wa Tume hiyo akiwemo Mhe.Balozi Omar Ramadhan Mapuri, ambaye ameteuliwa kwa kipindi cha pili, na Dkt.Zakia Mohamed Abubakar.
.
Uteuzi wa Wajumbe hao unaanza Julai 01, 2023.