Back to top

VYAMA VYA USHIRIKA VIMESAIDIA BEI YA MAZAO KUONGEZEKA

02 July 2024
Share

Mifumo ya Ushirika nchini imetajwa kusaidia bei za mazao mbalimbali ikiwemo zao la Kakao kuongezeka, ambalo limeongezeka kutoka wastani wa Tsh.7,000/= kwa kilo msimu wa 2022/2023, hadi wastani wa TSH. 29,000/= kwa kilo msimu wa 2023/2024.
.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde, wakati akifungua Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani, katika Viwanja vya Ipuli Mkoani Tabora, ambapo ameitaka Tume ya Maendeleo ya Ushirika pamoja na Taasisi nyingine zinazohusika na Ushirika kusimamia vyema uendeshaji wa Vyama vya Ushirika ili viweze kutumika kama nyenzo ya kuimarisha uchumi na kuondoa umasikini.
.
Amesema Serikali ina azma ya kuhakikisha inasimamia na kuimarisha Vyama  vya Ushirika ili viwasaidie Wananchi wengi kiuchumi kupitia Vyama vya Ushirika wa Kilimo na Masoko (AMCOS), SACCOS na Ushirika wa aina nyingine.
.
Kwa upande wake Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Benson Ndiege, ameeleza kuwa Tume hiyo itaendelea kusimamia Vyama kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu, ambapo ameendelea kuwaasa Viongozi wa Ushirika kuendesha Vyama kwa Uadilifu na weledi.